Viongozi watofautiana kuhusu hotuba ya rais Kenyatta


Viongozi mbalimbali wametoa hisia mseto kuhusiana na hotuba ya rais Kenyatta alasiri ya leo.

Kiranja wa wengi katika bunge la senate irungu Kang’ata amepongeza hotuba hiyo hasa kuhusiana na ahadi ya utoaji wa hati miliki zaidi za ardhi kwa wananchi.

Hata hivyo, mbunge wa Dagoretti kusini John Kiarie anasema kuwa rais Kenyatta hataeleza bayana yatakavyotekelezwa baadhi ya masuala aliyoibua hasa kuhusiana na vijana nchini.