VIONGOZI WASHIRIKIANE NA KUACHA SIASA ZA CHUKI, ILI KUTOA HUDUMA ZIFAAZO KWA WANANCHI ,LAMU.


Wito umetolewa kwa wanasiasa Lamu kusitisha mizozo waliyonayo kuhusiana na siasa za mwaka 2022, na badala yake kushirikiana kufanya kazi pamoja ili wakaazi waliowachagua wapate huduma zinazohitajika.

Mwakilishi wa wadi ya Hindi katika kaunti ya Lamu Anab Hajj amesema ,viongozi wanapoendelea kukosa kushirikiana ,wanawaumiza wananchi wa kawaida.

Katika kikao na waandishi wa habari Hajj ameeleza kuunga mkono HANDSHAKE akisema viongozi wa kaunti sawia na taifa kwa ujumla wanafaa kushirikianaili kuinua maisha ya wananchi.