VIONGOZI WAJITOKEZA KULAANI KISA CHA MWANAFUNZI KUPIGWA RISASI KILIFI.


Siku moja tu baada ya mwanafunzi wa darasa la sita kupigwa risasi na polisi mjini Malindi ,viongozi wa kaunti ya Kilifi sasa wamejitokeza na kulaani vikali tukio hilo .

wakiongozwa na Gavana wa Kilifi Amason Kingi ,ameisuta vikali idara ya polisi kwa kuchukua hatua hiyo kwa misingi kuwa mzozo wa ardhi ,haufai kusuluhishwa na bunduki.

Kingi ameshikilia kuwa tukio hilo limetekelezwa kinyume na sheria mna kwamba sharti swala hilo lifikishwe kwa mamlaka ya kuchunguza utendakazi wa polisi IPOA.

Kauli ya Kingi inajiri huku mwanafunzi huyo kwa jina Mbaga Lewa wa shule ya msingi ya Maziwani ,akiendelea kupigania uhai wake katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi.