VIONGOZI WAACHANE NA SIASA , NA KUANGAZIA MAENDELEO,KILIFI.


Viongozi katika kaunti ya Kilifi sasa wanatakiwa kuangazia maendeleo badala ya siasa , miongoni mwao.

Kulingana na katibu wa wizara ya barabara kaunti hiyo Ken Kazungu ,baadhi ya viongozi wanashiriki siasa zaidi badala ya kuhudumia wakaazi.

Kazungu amehoji kuwa wengi wa viongozi hao wanaingiza siasa kwenye miradi mbali mbali ya maendeleo, badala ya kutoa huduma zitakazo wafaidi wananchi.

Aidha Kazungu amehoji kuwa japo wizara hiyo inakumbwa na changamoto kadha wa kadha, kwa sasa imepiga hatua kubwa katika Nyanja ya miundo msingi, kinyume na inavyodaiwa na baadhi ya viongozi.

Kauli ya afisaa huyo inajiri siku chache tu .baada ya mwakilishi wa wadi ya Ganze Benson Chengo, kudai kwamba baadhi ya barabara katika kaunti hiyo zimekosa kuangaziwa.