Viongozi wa kiislamu walalamikia mauaji ya kiholela


Viongozi wa jamii ya kiislamu nchini imemtaka rais Uhuru Kenyatta kuingilia kati kuzima visa vya watu wanaouawa kiholela sawa na kupotea kwa njia tatanishi.

Viongozi hao kutoka mashirika kadha ya kiislamu wanadai kuwa baadhi ya watu nchini hasa waislamu wamekuwa wakitekwanyara na maafisa wa usalama kisha baadaye kupatikana wakiwa wameuawa suala linalowahuzunisha.

Vile vile wanaishinikiza serikali iangazie upesi maslahi ya wahudumu wa afya.