Vijana Lamu watakiwa kujifunza taaluma kuwawezesha kupata kazi za bandari.


Gavana wa kaunti ya Lamu Fahim Twaha ametoa wito kwa vijana wa Lamu kujiunga na vyuo ili wapate tahaluma mbalimbali zitakazowawezesha kupata nafasi za ajira katika bandari ya Lamu.

Kulingana na Gavana Twaha meli zitakapoanza kutia nanga katika bandari hiyo kazi nyingi zitapatikana ambazo zitahitaji vijana wa kufanya kazi hizo kama kupakia na kupakua mizigo.