Vijana kortini kwa kutotii


Mahakama Kisumu imeagiza Vijana watatu waliotiwa mbaroni katika nyumba moja eneo la Milimani kaunti ya Kisumu wakijivinjari wazuiliwe hadi kesho kesi yao itakaposikizwa.

Vijana hao wa kati ya umri wa miaka 18 na 21 wamekanusha kuwa wamekiuka masharti ya kuzuia covid-19 mbele ya hakimu mkuu Robinson Ondieki.

Mahakama imeambiwa kuwa vijana hao walifeli kuvalia maski na kuzingatia umbali wa mita moja unusu, watatu hao wakiitaka Mahakam iwaachilie huru kwa ahadi kuwa hawatakiuka masharti hayo tena.

Vijana hao walikuwa kati yaw engine 40 waliotiwa mbaroni katika eneo hilo lakini wenzao wakaachiliwa jioni ya jana katika kituo cha polisi cha Kisumu central kwa kuwa walikuwa chini ya umri wa miaka 18.