UTATA WA ELIMU KAUNTI YA TANA RIVER


Wizara ya elimu kaunti ya Tana River yashauri walimu wakuu wa shule za upili eneo hilo kutumia fedha za miundo msingi wanazopewa na serikali kutatua baadhi ya changamoto zinazojitokeza kufuatia ongezeko la wanafunzi kuambatana na mpango wa kuhakikisha wasnafunzi wote walionmaliza darasa la nane wanajiunga na shule za upili.

Tamko hilo linajiri wakati ambapo baadhi ya shule eneo hilo ikiwemo Ndura na Daku zimeripoti ongezeko la wanafunzi wengi kuliko idadi ya waliotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza huku Mkurugenzi wa Elimu, Joseph Nyaga, akisema walimu wakuu nwanastahili kutumia fedha inayotolewa na serikali ya miundo msingi kutatua changamoto inayojitokeza shuleni humo.

Licgha ya kampeni ambayo inaendelea kuhakikisha wanafunzi wanajiunga na kidato cha kwanza, shule nyingi za upili Tana River bado zinaripoti idadi ndogo ya wanafunzi kuliko wale wameitwa kujiunga na shule hizo huku baadhi ya wazazi wakiwatafutia watoo wao nafasi katika shule za kaunti ya Kitui na Kilifi.