USAMBAZAJI WA MAJI WARUDI , BAADA YA UKARABATI WA BOMBA LILILOPASUKA LA MZIMA KUAMILIKA-TAITA TAVETA.


Kampuni ya usambazaji maji ya Tavevo kaunti ya Taita Taveta imesema kwamba ,ukarabati wa bomba la Mzima lililopasuka siku ya alhamisi ,sasa limekamilika na usambazaji maji utarejelewa kama kawaida.

Haya yanajiri huku wakaazi wa mji wa Voi na maeneo mengine ya kaunti hiyo ,sawia na kaunti za Mombasa,Kwale na Kilifi ,wakikosa maji kufuatia kupasuka kwa bomba hilo.

Aidha maeneo mengine yaliyoathirika na uhaba huo wa maji, ni pamoja na gereza kuu la Manyani ambao wanategemea maji kutoka kwa bomba hilo la Mzima.