UKEKETAJI UKOMESHWE TAITA TAVETA.


Naibu gavana kaunti ya Taita Taveta Majala Mlaghui ametoa onyo kali kwa kina mama au jamii zinazoendeleza mila ya kukeketa wasichana , huku akiweka wazi kuwa wahusika wa watakabiliwa kisheria.
 
Majala anasema mtindo wa kuwakeketa watoto wachanga pia ni sharti ukome na kwamba watashirikiana na maafisa wa utawala wa mkoa kukabili mtindo huo.
 
Haya yanajiri huku kampeni kali ikiendeshwa kukabiliana na visa vya ukeketaji katika maeneo ya mipaka kaunti hiyo.