Uhuru na Raila wapokezwa ripoti ya BBI


Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga hatimaye wamepokezwa ripoti ya mwisho ya BBI.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa katika ikulu ndogo ya Kisii, rais Uhuru Kenyatta ameshabikia ripoti hiyo akihimiza wakenya kujisomea bila kutekwa kisiasa.

Ameitetea ripoti hiyo akisema haijaandaliwa kumlenga yeyote.

Naye kinara wa ODM Raila Odinga amesema kuwa changamoto zinzokabili maeneo tofauti ya humu nchini yameangaziwa katika mapendekezo ya ripoti hiyo.

Raila amewashtumu wanaopinga BBI akisema kuwa hawawatakii mazuri wananchi.

Raila amesema kuwa mapendekezo ya ripoti hiyo hayalengi kutoa nyadhifa za uongozi kwa wawili hao.

Ameelezea matumaini kuwa mapendekezo ya ripoti hiyo yataungwa mkono kikamilifu.