Uhaba wa majokofu changamoto kwa wafanyibiashara wa Samaki.


Wafanyibiashara wa kuuza samaki katika soko la samaki la Mji wa Kale kaunti ya Mombasa wametaja uhaba wa majokofu kama chngamoto kuu katika biashara hiyo.

Kulingana na Ali Fahmi Shikobo ambaye ni mfanyibiashara hatua hiyo inawatatiza na kupelekea hasara katika biashara zao huku wakilazimika kutumia mbinu zengine kuhifadhi samaki hao.

Ametaja kujitolea kwa baadhi ya wafadhili mbali mbali ikiwemo mbunge wa mvita  katika kuwapa motisha wafanyibiashara kama miongoni mwa sababu zinazopelekea biashara hio kunoga zaidi.

Wametaka changamoto hiyo kutatuliwa ili waweze kuendelea na biashara hiyo kwani wakati huu wa ugonjwa wa COVID biashara inazidi kukumbwa na changamoto.