Uhaba w chakula kwa vijana Kilifi.


Vijana kutoka eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, sasa wanalia ngoa kuhusu uhaba wa chakula wakati huu wakenya wanapokumbwa na janga la virusi vya Corona.

Katika taarifa kwa wanahabari chini ya uongozi wa Ali Maloseni, vijana hao wamelalama kuwa kwa muda sasa wamekuwa wakipitia wakati mgumu hasa baada ya wengi wao kupigwa kalamu kufuatia janga la Corona.

Kwa sasa wanatoa wito kwa viongozi wa serikali ya kaunti hiyo kuwaajiri angalau vibarua vya kutwa ikizingatiwa kwamba kufikia sasa wamesalia kuzurura ovyo mitaani.

Hata hivyo mwenyekiti wa kamati ya CDF eneo bunge la Magarini Samson Kombe, ameitaka serikali kuu kuongeza mgao wa fedha za mradi wa kazi mitaani unaolenga kuwaajiri vijana kutoka mashinani.

Kombe amefichua kuwa kwa sasa idadi ya waraibu wa mihadarati eneo hilo imeongezeka kufuatia ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.

Mwisho na Zomolo Wanje.