Uchaguzi mdogo wa Dabaso wazua tetesi


Huku tarehe ya uchaguzi mdogo wa wadi ya Dabaso kule kaunti ya Kilifi ikiwadia aliyekuwa mwakilishi wadi eneo hilo Emmanuel Changawa amepuzilia mbali tetesi kutoka kwa wagombea wenza kuwa tayari wamepewa cheti cha uteuzi wa ODM.

Kulingana na Changawa kauli hizo ni propaganda na kwamba sharti wapambane katika mchujo katika ODM.

Changawa anasisitiza kuwa hakuna mgombea atakayependelewa katika uteuzi wa ODM na kwamba kila mgombea sharti ashiriki uteuzi.

Fauka ya hayo Changawa amehoji kuwa endapo kutakuwa na mchujo basi sharti uwe wa huru na haki.

Changawa amesistiza kuwa ingekuwa vyema iwapo angepewa uteuzi wa moja kwa moja ikizingatiwa kwamba ametumia fedha nyingi wakati kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa mahakamani na mlalamishi Dickson Karani wa chama cha ANC.

Hata hivyo, baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa wako tayari kwa uchaguzi huo wakisistiza kuwa watachagua mtu binafsi na wala sio chama.