UA WA UMEME UNAFAA KUWEKWA KUSITISHA MIZOZO KATI YA WANYAMA PORI NA WAKAAZI, TAITA TAVETA.


Mizozo kati ya wanyamapori na binadamu kwenye kaunti ya Taita Taveta utapata suluhu iwapo shirika la kuhifadhi wanyamapori nchini litaweka ua wa umeme ili kuzuia wanyamapori kuingia makazi wa binadamu.

 
Mbunge wa Mwatate Andrew Mwadime anasema kamati inayohusika na masuala hayo katika bunge la kitaifa itawasilisha jibu juma lijalo , baada yake kuibua swali bungeni ili kufahamishwa na waziri wa utalii na wanyamapori kuhusiana na  hatma ya ua wa umeme ambao utazuia pakubwa wanyamapori kuwadhuru wakazi wa maeneo ya Mgeno, Gimba, Saghala, na Kasighau.
 
Aidha haya yanajiri huku mbunge huyo akiendelea kushinikiza serikali ya kitaifa kurejesha mbuga ya Tsavo kuwa chini ya usimamizi wa kaunti ya Taita Taveta.