TUME YA ARDHI ISULUHISHE MASWALA YA ARDHI.


Wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta wameitaka tume ya ardhi nchini kuharakisha kusuluhisha migogoro ya ardhi eneo hilo.

Kulinga na mwanaharakati Japhet Nyambu serikali ya kitaifa haijashuhulikia mizozo ya ardhi vilivyo huku ukosefu wa hati miliki ikiongeza swala la mizozo kuzidi hata zaidi.

Amesema kuna haja kwa mabunge ya kaunti ukanda wa pwani kubuni sera zitakazosaidia kusuluhisha mizozo ya ardhi.