Tuju akiri Mungu ni wa ajabu


Katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju, amezungumza kwa mara ya kwanza tangu ahusike katika ajali ambayo ilimfanya kupata majeraha mabaya.

Tuju ambaye pia ni waziri asiye na majukumu, amezungumza katika mkao na waandishi wa habari Karen Hospital hapa Nairobi akiandamana na daktari wake mkuu Dan Gikonyo, huku akisema alipata majeraha mabaya sana.

Tuju alihusika katika ajali mwezi jana akiwa safarini kwenda Kabarak kaunti ya Nakuru, kuhudhuria mazishi yake rais mustaafu Daniel Toroitich arap Moi.

Baada ya ajali hiyo alisafirishwa kupelekwa London nchini uingereza kwa matibabu maalum, kabla ya kurejea nchini juzi.

Anasema kuwa ni Mungu tu aliyempa nafasi nyingine maishani hasa baada ya kunusurika katika ajali ya ndege Busia mwaka wa 2003.