Taita taveta kushirikiana kwa ajili ya wagonjwa wa Saratani .


Serikali ya kaunti ya Taita Taveta itashirikiana na mashirika mbalimbali kuhakikisha wagonjwa wa saratani wanapata matibabu kwa wakati ufaao.

Kulingana na waziri wa afya kaunti hiyo John Mwakima anasema changamoto ya kifedha miongoni mwa wagonjwa hao ni jambo ambalo wameanza kulifikiria na kwamba watasaidia katika matibabu hayo.

Hata hivyo waziri huyo amesema wataanza kutoa bima ya matibabu kwa jamaa ambao hawajiwezi katika jamii.