SUALA LA ARDHI LISHUHUKIWE VOI


Wakaazi wa Voi kaunti ya Taita Taveta wanalalamikia unyakuzi wa ardhi za rasilimali za umma, hatua wanayodai kutekelezwa na baadhi ya mabwenyenye mjini humo.

Wakaazi hao wanadai baadhi ya watu wamekuwa wakinyakuwa vipande vya ardhi zilizotengewa shughuli za kimaendeleo, huku ardhi za shule zisizo na hati miliki zikitajwa kuathirika zaidi.

Kwa sasa wanatoa wito kwa tume ya ardhi sawa na serikali ya kaunti kuingilia kati ili mwafaka uweze kupatikana.