Sita wanusurika kifo Likoni.


Watu 6 wamepata majeraha baada ya kuhusika katika ajali eneo la Kindunguni barabara ya Likoni Lungalunga katika eneo la Likoni Jana jioni.

Ajali hiyo imehusisha Lori lililokuwa likielekea upande wa feri na matatu iliyokuwa ikielekea upande wa Ukunda.

Aidha walioshuhudia wanasema kuwa Lori hilo na matatu ziligonganana ana kwa ana.

Majeruhi walipelekwa katika hospitali ya karibu ambapo baadhi yao walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.