Simba wavamia kijiji cha Changoto Kilifi


Hali ya wasi wasi imezagaa katika Kijiji cha Changoto Adu kaunti ya Kilifi baada ya jumla ya simba watatu kuvamia eneo hilo na kushambulia mifugo.

 

Katika taarifa kwa wanahabari chifu wa eneo hilo Patrick Charo, amedokeza kuwa tayari wanashirikiana na shirika la huduma kwa wanyama pori nchini KWS kuwasaka simba hao.

 

Charo ameshikilia kuwa hali hiyo imewatia hofu wanafunzi wanaorauka kwenda shuleni ikizingatiwa kuwa maficho yao hayabainika.

 

Amewataka wenyeji wa sehemu hiyo kuwa makini zaidi hususan nyakati za usiku.

 

Ameongeza kuwa huenda hayawani hao wamefika eneo hilo kutokana na ujio wa wafugaji wa kuhamahama ambao pia wamepiga kambi eneo hilo.

 

Hata hivyo afisaa mkuu wa shirika la KWS tawi la Malindi na Magarini Jane Gitau, amehoji kuwa tayari wameweka mitego ya kuwanasa simba hao.