Sijutii kutimuliwa,Duale adokeza


Mbunge wa Garissa mjini Adan Duale anasema kuwa anaondoka kutoka wadhifa wa kiongozi wa wengi akiwa mchangamfu kutokana na mengi aliyotekeleza kuu ikiwa kupitishwa kwa zaidi ya miswada 200 na hoja 500.

Duale ameambia bunge kuwa kamwe hajutii kuondolewa wkake na kwamba kamwe hatakuwa na kisasi na mtu kwa hatua hiyo.

Katika hotuba ambayo amesema ni ya kusema kwaheri kutoka wadhifa huo, Duale amewaomba masamaha wote aliowakosea alipokuwa usukani.

Duale alitemwa jana katika mkutano wa muungano wa wabunge wa Jubilee nafasi yake ikijazwa na mbunge wa kipipiri Amos Kimunya.

Kimunya ameshabikia uongozi wa Duale bungeni na kuhimiza wabunge kushirikiana kuhakikisha ajenda ya chama cha Jubilee inafanikishwa.