SHULE ZINAZOJENGWA ZIZINGATIE UBORA-TAITA TAVETA.


Ipo haja ya washikadau mbali mbali wa elimu ambao wanaendeleza ujenzi wa miradi ya shule, kuzingatia kikamilifu maagizo ya idara ya ujenzi, ili kukidhi mahitaji kwa watumizi hasa wenye ulemavu.

Haya ni kwa mujibu ya walimu wakuu kwenye shule za kaunti ya Taita Taveta ,ambao wametolea mfano wa majengo ya orofa eneo bunge la Mwatate kwa shule za msingi za Mwakinyungu, Dembwa , Mazola na Mulughi ..yaliyojengwa kwa fedha za ustawi wa maeneo bunge ,CDF eneo bunge la Mwatate .

Wanasema shule hizo zimejengwa kwa ubora ,zikizingatia maslahi ya wanafunzi na walimu wenye ulemavu wa kutembea, kwani wahusika wanaweza kuyafikia madarasa kupitia viti vyao maalum