Shule za upili zimejaa hadi pomoni


Shule za upili nchini kwa sasa hazina uwezo wa kuhimili uwezo wa kuwapa hifadhi wanafunzi wote.

Mwenyekiti wa muungano wa wakuu wa shule za upili nchini Kahi Indimuli anasema kuwa shule nyingi nchini hazina miundo msingi ya kutosha kuwawezesha wanafunzi wote wa kutoka kidato cha kwanza hadi cha nne kuzingatia masharti ya wizara ya afya.

Katika mahojiano na Radio Citizen ndani ya mjadala wa Jambo Kenya, Indimuli amesema kuwa walimu wamekuwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha wanafunzi wanazingatia masharti ya kuzuia maambukizi ya Covid-19.