SHULE NYINGI KATIKA MSITU WA BONI ZAKOSA KUFUNGULIWA KUTOKANA NA CHANGAMOTO ZA KIUSALAMA-LAMU


Wanafunzi wa chekechea hadi darasa la nne ,katika maeneo yaliyo ndani ya msitu wa Boni kaunti ya Lamu, wamekosa kufika mashuleni mwao tangu shule kufunguliwa, kufuatia kuchelewa kwa walimu kufika maeneo hayo.

Walimu katika maeneo hayo wanalazimika kusafirishwa kutumia ndege ya jeshi au polisi, kwani usafiri wa barabarani unahatarisha maisha yao, ikizingatiwa kwamba ni maeneo ambayo yanaendeleza Oparesheni dhidi ya magaidi wa Alshabab .

Wanafunzi hao wataanza masomo yao rasmi kuanzia juma lijalo ,ambapo tayari walimu wametumwa maeneo yao na Idara ya usalama hii leo.

Kwa wanafunzi wa darasa la tano hadi darasa la nane wa maeneo hayo ya Boni ,tayari wamesafirishwa katika shule ya msingi wanayosomea ya Mokowe Arid Zone ,Kwa kutumia ndege ya jeshi ,baada ya kuchelewa kufika shuleni kwa muda wa juma moja.