Shirika moja la kijamii lataka lango kuu la hospitali ya Makadara kufunguliwa.


Shirika moja la kijamii limeelekea mahakamani kuishurutisha kaunti ya Mombasa na usimamizi wa hospitali kuu kanda ya Pwani kufungua lango kuu la hospitali hiyo kwa umma.

Haya yanajiri baada ya lango hilo kufungwa mnamo mwezi Machi mwaka huu katika juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19.