SHIRIKA LA KENYA FERRY LAPUUZILIA MBALI MADIA YA KUSITISHA ABIRIA KUVUKA


Shirika la Kenya limepuuzilia mbali taarifa zilizokuwa zinaenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba abiria wanaotumia Ferry kule Likoni wataruhusiwa kuvuka tu kwa kutumia magari pekee na wala sio kwa miguu.

Kwenye taarifa hio, shirika la Kenya ferry limesema kwamba halijapokea barua yoyote kutoka kwa waziri inayowaagiza kutekeleza madai hayo na kushikilia shughli zote zinaendelea kama kawaida katika kivuko hicho huku abiria wakihimizwa kuvaa Barakoa na kila mmoja kuwa na mwenzake umbali wa mita moja na nusu.

Awali baadhi ya abiria wanaotumia kivuko hicho walikuwa wameelezea hofu ya kutumia magari pekee kwenye kivuko hicho wakisema kwamba ni hatua ambayo ingechangia msongamano mkubwa wa magari.

Haya yanajiri huku Rais Uhuru Kenyatta akiagiza maafisa wa Coast Guard na Kenya police kuchukua usukani wa kudhibiti abiria wanaotumia kivukocha likoni Ferry.