Shirika la KEBS laonya wakenya dhidi ya vieuzi


Je, unafahamu iwapo vieuzi au sanitizers unazotumia ni zinazofaa?

Shirika la kikadiria ubora wa bidhaa nchini KEBS limeonya wakenya dhidi ya kununua au kutumia sabuni hizo za kuua viini bila kuthibitisha uhalali wazo.

Mkurugenzi wa ubora katika shirika hilo Bernard Nguyo ameambia Radio Citizen kuwa kuna wafanyibiashara walaghai wanaowauzi wakenya vieuzi visivyofaa.

Amewataka wakenya kuwa waangalifu zaidi.