SERIKALI YAWAACHILIA WAGONJWA-TAITA TAVETA


Ni afueni kwa wagonjwa wenye afueni katika hospitali za umma kaunti ya Taita Taveta na  ambao wamekuwa wamezuiliwa kwa kukosa fedha kwani sasa wanaeza enda nyumbani.

Kulingana na gavana wa kaunti ya Taita Taveta Granton Samboja anasema hatua hiyo ni moja wapo ya kupunguza idadi ya juu ya wagonjwa katika hospitali za umma wakati huu virusi vya Corona vinatatiza taifa hili.

Haya yanajiri huku pia maafisa wa afya wakizuru hoteli mbalimbali za kitalii katika mbuga ya Tsavo mashariki kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa kiafya kwa wafanyikazi wa hoteli hizo.