Serikali yajitetea kwa kuendelea kufungia kaunti tano


Serikali imetetea hatua yake ya kuongeza muda wa marufuku ya kutoingia na kutoka kaunti tano nchini, Nairobi, Mombasa, Kilifi, Kwale na Mandera

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna anasema hatua hiyo imesaidia pakubwa kupunguza maambukizi, akisema ilivyo kwa sasa, maambukizi mengi ni kutoka Nairobi na Mombasa

Ameyasema haya baada ya Nairobi na Mombasa kuandikisha idai ya juu ya maambukizi jana, ambapo kati ya watu 57 waliothibitishwa kuwa na COVID-19, 35 walitoka Mombasa, 17 wakiwa kutoka hapa Nairobi