Serikali ya kitaifa kuanza mpango wa kutoa chakula kwa waathirika wa mafuriko Tana River.


Serikali ya kitaifa kaunti ndogo ya Tana River yaanza mchakato wa kutoa chakula kwa familia 627 ambazo zimefurushwa makwao na mafuriko baada ya mto tana kuvunja kingo zake na wanaishi katika kambi za muda kwa sasa.
Utoaji chakula umeanza rasmi kwa waathirika wa mafuriko kutoka mtaa wa Mwangaza mjini Hola ambao pia wamepata magodoro, gunia la mchele la kilo 50 kwa kila familia sawia na dawa za kusafisha maji na kieuzi kwa ajili ya kuosha mikono kupambana na ugonjwa wa virusi vya Corona.
Msaidizi wa Kamishna wa kaunti, Geoffrey Mwachofi, akiongea kwa niaba ya Naibu Kamishna wa kaunti ndogo ya Tana River, anasema kila kambi itapata ya waathirika wa mafuriko itapata chakula na misaada mengine kutoka kwa serikali.
Mmoja ya waathirika wa mafuriko, Elizabeth Malika anasema msaada huo utasaidia pakubwa japo bado anasisitiza serikali kuwatafutia ardhi mbadala ambapo wanaweza kuweka makazi ya kudumu.