SERIKALI KUTENGA ENEO MPYA KWA WAGONJWA WA COVID 19 TAITATAVETA.


Serikali ya kaunti ya Taita Taveta iko mbioni kuweka mahala maalum kwa wagonjwa wa virusi vya Corona katika chuo cha CIT mjini Voi.
 
Kulingana na gavana Granton Samboja jumla ya vitanda 160 vitawekwa eneo hilo ili kuhakikisha wagonjwa wa Covid 19 hawatangamani na jamii.