SERIKALI KUHUSU UGONJWA WA SARATANI-TAITA TAVETA.


 

Kuna haja kwa serikali kuondoa ushuru kwa dawa zinazotibu ugonjwa wa saratani ,kwani wagonjwa wengi wanazidi kuumia mashinani.

Kulingana na aliyekuwa mwakilishi wa wanawake kaunti ya Taita Taveta Joyce Lay anasema ,kufikia sasa kuna haja kwa mikakati kuwekwa na serikali za kaunti sawIa na ya kitaifa ,ili kuhakikisha wagonjwa hao wanapata matibabu bila malipo.

Vile vile Lay anasema kuna haja kwa hamasa kufanywa mashinani, ili wanawake waweze kufanyiwa uchunguzi wa saratani kwa wakati ufaao.