SERIKALI IZINGATIE KIKAMILIFU ELIMU YA BURE PINDI SHULE ZIKAPOFUNGULIWA LAMU.


Serikali kuu imetakiwa kuanzisha mpango wa elimu ya bure kikamilifu pindi shule zitakapofunguliwa ili kuwasaidia wazazi ambao wengi wanakabiliwa na hali ngumu za kimaisha baada ya kuathirika na janga la korona.

Mwanaharakati wa kijamii katika kaunti ya Lamu Issac Abubakar amesema wazazi wengi kwa sasa hawana ajira na wengine wengi kusalia majumbani baada ya kutimuliwa kazini tangu korona kubisha hodiĀ  nchini.

Abubakar amesisitiza kuwa janga la korona ni sababu tosha serikali kuu inapaswa kuzingatia na kuanzisha elimu ya bure kwa wanafunzi ili kusaidia wazazi na fedha za karo.