SERIKALI IWE IMARA KATIKA SWALA LA VITAMBULISHO,TANA RIVER.


Serikali inastahili kuwa imara na kuhakikisha zoezi la utoaji vitambulisho kaunti ndogo ya Tana Delta haikumbwi na utata na sintofahamu ili wakazi wa eneo hilo wapate stakabadhi hiyo mkuhimu ya kitaifa.
Gavana Dhadjo Godhana, asema swala la utoaji vitambulisho Tana Delta hukumbwa na utata mara kadhaa na kamati ya usalama eneo hilo inastahili kuwa ngangari zaidi ili kuhakikisha wakazi wa eneo hilo pekee ambao wanastahili kupata kitambulisho ndio wanapata.
Ametoa wito kwa idara ya usajili wa watu kuhakikisha wanaongeza muda wa usajili wa vitambulisho kwa wakazi eneo hilo kwani kuna idadi kubwa ya vijana wamefikisha umri wa kupata vitambulisho na hawajapata.