SERIKALI IINGILIE KATI , WANANCHI WANUFAIKE NA RANCH TAITA TAVETA.


Huku mdahalo ukiendelea kuhusu umiliki wa mashamba makubwa ya kukodi kaunti ya Taita Taveta,sasa wito unatolewa kwa serikali kuingilia kati ili wananchi waweze kunufaika na mashamba hayo.

 
Kulingana na mwanaharakati Mnjala Mwaluma anasema kufikia sasa baadhi ya mashamba hayo muda wake wa kukodi umekamilika ila watu wachache wanajaribu kadiri ya uwezo wao kutohusisha mwananchi.
 
Mnjala anasema kwa sasa mizozo baina ya wafugaji na wakulima imechangiwa na watu wachache ambao wanakodisha bila kufuata taratibu mwafaka.