SENETA WA TAITA TAVETA APINGA MSWAADA WA KUPUNGUZIWA FEDHA KWA KAUNTI.


Seneta was kaunti ya Taita Taveta Jones Mwaruma amesema kwamba sharti fedha zinazoelekezwa katika serikali za kaunti zisipungizwe.

Mwaruma anasema kaunti ya Taita Taveta huenda ikapoteza shilingi bilioni moja iwapo mswaada wa ugavi wa raslimali ambao uko katika bunge la seneti utapitishwa jinsi ulivyo.
Mwaruma vilevile amelalamika jinsi serikali ya kitaifa inavyo orodhesha kaunti kame akisema kaunti ya Taita Taveta ni miongoni mwa kaunti zilizoachwa nyuma kimaendeleo ila imeachwa nje.
Haya yanajiri huku gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja akisema huenda ikawa vigumu kutekeleza miradi ya maendeleo iwapo mswaada huo utapitishwa.