Ruto na Mudavadi wataka mdahalo kuhusu BBI


Naibu rais William Ruto amewataka viongozi walio na misimamo mikali kuhusu ripoti ya BBI kuilegeza ili kuwe na mazungumzo kuhusu masuala ibuka katika ripoti ya BBI.

Akizungumza katika kaunti ya Tharaka Nithi, Ruto amesema kuwa mdahalo komavu ndio njia ya pekee itakayosaidia taifa kuzungumza kwa sauti moja kuhusu mapendekezo ya BBI.

Anasema kuwa mdahalo wa kitaifa utasaidia kuepushia taifa gharama kubwa ya kuandaa kura ya maamuzi.

Kauli sawia imetolewa na kinara wa ANC Musalia Mudavadi aliyeuwa kizungumza katika kanisa la Ngong Salvation Army kaunti ya Kajiado.