Ruto asusia hafla ya BBI


Rais uhuru kenyatta na kinara wa Odm Raila odinga walipokuwa wakipokea ripoti ya BBI Naibu rais William Ruto alikuwa eneo la Eldoret kaunti ya Uasin Gishu katika hafla ya mazishi ya aliyekuwa mwakilishi wadi ya Huruma Peter Chomba.

Maoni mbalimbali sasa yakitarajiwa baada ya ripoti hiyo kutolewa kwa umma.

Seneta wa Elgeyo marakwet Kipchumba Murkomen kupitia ujumbe wa tweeter amesema kama ilivyotarajiwa si yakuridhisha huku tayari akianza kuikosoa na kusema kuwa wanaopendekeza maseneta wawili kwa kila kaunty hawafahamu vema ugatuzi.

Murkomen anashangaa maseneta wawili watakuwa na majukumu yapi kwa kuwa kila seneta ana kura moja inayowakilisha kaunty.