Ruto asisitiza mwanya wa mazungumzo kuhusu BBI


Naibu rais William Ruto amewashtumu viongozi wanaopuzilia mbali wito wa kuwa na maswali kadhaa yatakayoangaziwa katika kura ya maamuzi kuhusu mabadiliko ya katiba.

Akizungumza Narok katika hafka ya mazishi ya katibu msaidizi katka wizara ya Leba Patrick Ole Ntutu,Naibu rais amekariri haja ya masuala tata yabadilishwe sasa kabla ya kura ya maamuzi kuandaliwa.

Viongozi mbalimbali hasa wanaoegemea upande wa naibu rais William Ruto wameshabikia ushindi wa mgombea huru katka uchaguzi mdogo eneo bunge la Msambweni Feisal Bader hapo jana wakisema unaashiria mema kisiasa katika uchaguzi mkuu mwaka wa 2022.

Wakiongozwa na gavana wa Bomet Hillary Barchok, mbunge wa Narok kusini Korei Ole Lemein na mbunge wa kaunti ya Narok Soipan Tuya, viongozi hao wamesema kuwa ushindi wa hapo jana unaipa kambi ya Ruto uwezo zaidi kisiasa.

Kauli yao imeungwa na mbunge wa Mumias Mashariki  Benjamin Washiali na mwenzake wa Kiharu Ndindi Nyoro ambao wamesema kuwa ushindi wa hapo jana ni kiashiria kuwa BBI haitapata mwanya iwapo masuala tata yatapuuzwa na waasisi wake.