Rubani anaswa kwa kuhusishwa na sakata ya silaha


Subow Mohamed Ahmed anayehudumu kama rubani katika kampuni moja ya ndege humu nchini ametiwa mbaroni kuhusiana na  madai ya sakata ya shilingi bilioni 39 za silaha za kijeshi.

Idara ya upelelezi nchini DCI inasema kuwa mshukiwa amenaswa na maafisa wa usalama katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo kenyatta hapa nairobi.

Anahusishwa na madai ya sakata hiyo ambayo pia imemhusisha aliyekuwa waziri wa michezo Rashid echesa na washukiwa wengine watatu.

Echesa alishtakiwa mahakamani tarehe 17 mwezi jana akiwa na Daniel Otieno Omondi , Clifford Okoth Onyango na Kennedy Oyoo Mboya.