RIPOTI YA UHAKIKI WA SERIKALI KUU NA ZA KAUNTI-MOMBASA.


Huku kamati ya uhakiki wa maendeleo barani Afrika ikiendelea kuelimisha wananchi kuhusiana na ripoti kuhusu uhakiki hapa nchini ,wito umetolewa kwa serikali za kaunti kushirikina na kamati hiyo, ili wapate kuhakikiwa kulingana na kazi zao wanazofanya.

Akiongea mjini Mombasa mkurugenzi wa kamati hiyo humu nchini Dkt. Elias Mbau amesema kuwa ,ni muhimu kwa ushirikiano huu ili kaunti hizo ziweze kuhakikiwa kimaendeleo hasa baada ya baadhi ya majukumu kugatuliwa.

Mbau ameongeza kuwa Kenya imekuwa miongoni mwa mataifa barani Afrika ,ambapo wameweza kuafikia baadhi ya malengo ya maendeleo katika ruwaza ya mwaka 2030.

Kwa upande wake naibu waziri wa fedha Nelson Gashuhe ameisistiza kuwa sio mashindano kati ya kaunti lakini ni muhimu kwa uhakiki hasa ikilinganishwa kuwa ripoti ya mchakato wa BBI, inapendekeza fedha zinazotengewa kaunti kuongezwa hadi asilimia 35.

Mnamo kati ya mwaka 2016 / 2017 Kenya ilikuwa nchi ya kwanza kuhakikiwa barani Afrika ,huku ikitajwa kupiga hatua katika sekta mbali mbali ikiwemo huduma bora.