Rambi rambi kwa aliyekuwa mbunge wa Kilifi Kusini Mustaffa Iddi.


Risala za rambi rambi zinaendelea kutumwa kwa ndugu jamaa na marafiki wa aliyekuwa mbunge wa kilifi kusini Mustaffa Idi
Idi aliaga dunia mapema leo baada ya kuugua kw amda mfupi katika hospitali moja hapa mjini Mombasa

Marehemu anatarajiwa kuzikwa baaday ehii leo kwa mjibu wa taratibu za dini y akiislamu.

Kulingana na ndugu yake, Amir Matsaki Chikotero, Mustafa mwenye umri wa miaka 50, amekuwa hospitalini kwa kipindi cha siku 10, na kwamba ameaga leo asubuhi baada ya hali yake kuwa mbaya kuanzia usiku.

Iddi atazikwa nyumbani kwake katika eneo la Bomani Kikambala, huko Kilifi.

Katika uchaguzi wa mwaka 2017, Iddi aliwania tena kiti cha ubunge cha Kilifi kusini kwa tiketi ya Jubilee lakini akashindwa na Ken Chonga.