Rais Uhuru kuongoza hafla ya kufuzu kwa makurutu wa jeshi


Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza hafla ya kufuzu kwa wanajeshi wapya wa kikosi cha tisa hii leo

Hafla hiyo itafanyika katika uwanja wa chuo cha mafunzo ya kijeshi mjini Eldoret

Hata hivyo, idara ya jeshi KDF, imesema hafla hiyo haitakuwa wazi kwa umma kutokana na janga la Corona, familia za wanajeshi hao wakitakiwa kufuatilia tu hafla hiyo kwenye runinga na mitandao ya kijamii