Rais Uhuru asema hana nia ya kulivunjilia mbali bunge, alivyoshauri Maraga

Rais Uhuru Kenyatta ameeleza kuwa hana nia yoyote ya kulivunjilia mbali bunge kwa mujibu wa ushauri wa jaji mkuu David Maraga
Katika mahojiano na Runinga ya France24, rais ameeleza kuwa hata bunge likivunjiliwa mbali itasalia kuwa vigumu kuafikia usawa wa jinsia
Aidha ameonya kuhusu kampeni za mapema akimlenga naibu wake William Ruto, anayesema hajabatilisha uamuzi wake wa kumuunga mkono
Hata hivyo anasema wakati ukifika, ataeleza kuhusu anayemuunga mkono kikamilifu
Pia rais amesema Kenya haitaruhusu ndege zisizo na rubani au drones za Marekani katika anga za Kenya kutekeleza mashambulizi dhidi ya kambi za makundi ya kigaidi nchini Somalia
Ameongeza kuwa Marekani haijawasilisha ombi la kutaka kutumia ndege hizo na pia Kenya haioni haja ya kuwepo kwa ndege za aina hiyo