Rais azindua idara ya utekelezaji wa mtaala


Rais Uhuru Kenyata amesema kuwa serikali imeunda idara maalum serikalini itakayokuwa na jukumu la kuangazia mageuzi katika mtaala wa elimu nchini.

Idara hiyo itakuwa chini ya wizara ya elimu nchini.

Rais Kenyatta anasema kuwa idara hiyo itashirikiana na wadau husika ikiwemo tume ya kuwaajiri walimu nchini kufanikisha utekelezaji wa mtaala mpya wa elimu ikiwemo kuwapa mafunzo zaidi walimu nchini.

Ameelezea haja ya wanafunzi kupewa elimu zaidi hasa kuhusu ubunifu ili kuwa na nafasi bora ya kutemba maishani.