RAILA NA VIONGOZI WA KIISLAMU KUHUSU MASWALA YA KUUNGA MKONO BBI AKIWA MOMBASA.


Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga amekutana na baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu katika juhudi ya kupigia debe mchakato wa BBI katika kaunti ya Mombasa.

Akizungumza baada ya kukutana na viongozi hao ,Raila amesema kuwa wataendelea kushirikiana kuona baadhi ya mapendekezo waliyoyatoa yanaangaziwa hata siku za usoni.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza kuu la ushauri la waislamu Sheikh Juma Ngao, amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kuhakikisha kuwa wanabadilisha baadhi ya maswali waliyoyapendekeza.

Haya yanajiri siku moja tu baada ya uzinduzi wa shughuli ya kukusanya sahihi ya kuunga mkono mchakato huo, kaunti ya Mombasa.