Raila awashutumu wanaopinga mabadiliko ya katiba


Kinara wa ODM  raila odinga amewasuta wanaopinga katiba kufanyiwa marekebisho.

Akizungumza akiwa eneo la Mabole eneo bunge la Butere nyumbani kwake gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya, Raila amewahimiza viongozi kuunga juhudi za mabadiliko ya katiba akisema hatua hiyo inalenga kunufaisha wananchi .

Kwa upande wake Gavana Oparanya ameahidi kupigia debe kura ya maamuzi baada ya ripoti ya BBI kuwekwa wazi kwa umma.

Kauli iliyoungwa na mbunge wa Shinyalu Justus Mugali Kizito.