Raila akanusha kupigwa chenga katika BBI


Kinara wa ODM Raila Odinga amesema kuwa anaunga mkono kikamilifu ripoti ya BBI licha ya baadhi ya mapendeekzo yake kutojumuishwa katika ripoti ya mwisho.

Katika taarifa, Raila amesema kuwa kuwa ana ufahamu tosha kuhusu mabadiliko kadha yaliyofanyiwa ripoti ya mwisho.

Kauli yake inatokana na lalama kutoka kwa baadhi ya watu kuwa suala la kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC halikuwekwa bayana alivyotaka.

Anasema kuwa hatua hiyo haifai kutumiwa na baadhi kupinga ripoti ya BBI.