POLISI WAKAMATA WEZI SUGU HUKO KINONDO ENEO LA KILOLE.


Hatimaye idara ya usalama katika eneo la Msambweni imefanikiwa kuwakamata washukiwa watatu Sugu wa wezi katika kijiji cha kilole huko Kinondo eneo la msambweni kaunti ya Kwale.

Washukiwa hao walio wa miaka kati ya 14 hadi 17 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la kihalifu la rockstam, linaloaminika kuendeleza wizi na uhalifu katika kijiji cha kilole ,Zigira na Mwaweche, walikamatwa wakiwa wamejihami kwa mapanga,visu na silaha nyingine Butu tayari kutekeleza uhalifu.

Washukiwa hao ni pamoja na Juma Hassan ,Tubwa, na Sadik aliyetoroka korokoroni ,anayeendelea kusakwa na maafisa wa polisi huku wenzake wakisalia korokoroni kwa uchunguzi zaidi.

Kukamatwa kwa washukiwa hao kunajiri baada ya wenyeji katika kijiji cha Kilole kulamimikia utovu wa usalama katika eneo hilo, kwa zaidi ya miaka miwili sasa ,bila ya polisi kuchukua hatua zozote.